HUDUMA ZA TAFSIRI

Lugha
Kwa sasa, huduma hii inatolewa katika lugha mbili, ambazo ni Kiingereza na Kiswahili. 
Namna ya Kutafsiri 
Wanaisimu mahiri (Kiswahili & Kiingereza) wataitafsiri matini kwa kutumia tafsiri ya mwanadamu (kwa kiasi kikubwa) ili kuepuka makosa ya kisarufi yanayoweza kusababishwa na tafsiri ya mashine.

Pia, kusoma prufu kutafanyika kwa matini nzima kabla ya kuwasilishwa kwa mteja. Hii itafanyika ili kulinda  ubora wa matini.

Usiri
Suala hili ni muhimu sana katika taaluma yetu (Tafsiri). Wafasiri wetu wataihifadhi nyaraka yako katika hali ya usalama.

Bei
Bei ya kuridhisha imepangwa kulingana na aina ya matini.
Kwa sasa, matini zitatafsiriwa kutoka katika nyanja zifuatazo:


$ 0.19 kwa neno (Dola za Kimarekani). Bei hii ni kwa matini kutoka nyanja zifuatazo:
Isimu, Utawala, Utaliii, Elimu, Siasa, Michezo na Burudani, Masuala ya Kijamii, Historia, Vifaa vya Nyumbani, Sanaa, Bidhaa za Kawaida 

$ 0.25 kwa neno (Dola za Kimarekani). Bei hii ni kwa matini kutoka nyanja zifuatazo: 
Biashara, Kompyuta, Masoko, Muziki, Usafiri, Majengo, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

KUMBUKA 

Kama una matini ambayo haimo katika orodha ya matini zilizoorodheshwa hapo juu, tafadhali usisite kuwasiliana nasi ili  kuangalia  uwezekano wa kuitafsiri.

Tutumie oda yako kupitia: ulingokiswahili@gmail.com
                              au 
 Bofya hapa ili kusoma kwa Kiingereza