Hii ni wale Wanaojifunza Kiswahili kama Lugha ya Pili.
Bofya Kiunganishi hiki ili Kujifunza Sauti za Kiswahili kwa Kutumia Sauti na Picha. Hakuna Malipo!
_______________________________________________________________________
Walengwa
wa huduma hii ni wale wanaotaka
kujifunza Kiswahili kama lugha ya kwanza, ya pili au ya kigeni. Mjifunzaji
yoyote anakaribishwa kujifunza Kiswahili nasi.
Huduma
hii inapatikana kwa njia mbili, ambazo ni: njia ya ana kwa ana na njia ya
mtandao.
Njia ya Ana kwa Ana
Huduma
hii inatolewa kwa wajifunzaji wanaoishi Tabora (Tanzania). Kama unakaa katika
eneo hili au jirani, tafadhali usisite kuwasiliana nasi ili ujifunze lugha ya
Kiswahili ambapo utaweza kuwasiliana na Watanzania kikamilifu.
Bei ya Vipindi kwa Njia
ya Ana kwa Ana
Bei
ni Dola za Kimarekani Ishirini (20 USD)
kwa saa, kwa wajifunzaji wasio
Watanzania, na Shillingi za Kitanzania elfu kumi (TSH 10,000/=)
kwa kipindi kimoja kwa wajifunzaji ambao ni Watanzania.
KUMBUKA:
Inapendekezwa kutumia saa mbili za kujifunza na mazoezi.
Kama unahitaji hii
huduma katika kategoria hii, wasiliana nasi kupitia: ulingokiswahili@gmail.com
Njia ya Mtandao
Njia
ya pili ni ya mtandao. Huduma hii inatolewa kupitia Skype au mitandao mingine ambayo inaruhusu mawasiliano ya sauti na
picha.
Bei ya Vipindi kwa Njia
ya Mtandao
Kwa
wajifunzaji wa kiwango cha awali, bei yake ni Dola za Kimarekani 30 kwa saa.
Inapendekezwa kujifunza kwa saa mbili
ili kuwa na mazoezi ya kutosha.
Pia,
katika kategoria hii, mwalimu ataanza kutambulisha sauti za Kiswahili kwa
kutumia njia tofauti ili kuhakikisha mjifunzaji anazimudu sauti kirahisi.
Kwa
wale wenye msingi wa lugha ya Kiswahili (Wajifunzaji
wa kiwango cha kati na juu), na wanataka kufanya mazoezi ya uzungumzaji ili
kuimarisha uwezo wao, bei yake ni Dola
za Kimarekani 25 kwa saa.
KUMBUKA:
Unapoomba kama mjifunzaji wa kiwango cha kati au juu, hakikisha unao msingi wa lugha ya Kiswahili.
Muda wa Kujifunza
Makubaliano
yatafanywa kati ya mwalimu na mjifunzaji kuhusu muda wa kujifunza. Hakuna muda
maalumu uliopangwa kutokana na utofauti
wa muda sehemu mbalimbali za Dunia.
Tuma
maombi yako ya kujifunza kwa njia ya mtandao kupitia: Samahani, huduma ya kujifunza kwa njia ya mtandao haipatikani kwa sasa.